Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:52 pm

NEWS: MFAHAM MBUZI ANAYEKULA NYAMA NA MAANDAZI NA CHAI +VIDEO

NJOMBE: Mzee mmjo anayefahamika kwa jina la Antony Mwandulami (mganga wa kienyeji) ambaye ni mkaazi wa Mkoa wa Njombe ambao zamani ulikuwa sehemu ya mkoa wa Iringa anafuga mbuzi anayefanya kazi ambazo huenda zinafanana kwa kiasi fulani na zabinaadamu kama vile kumlindia nyumba yake, kumpa taarifa, kumfanyia kazi ndogo ndogo.

Anasema mbuzi huyo alie mpa jina la Damas amekuwa naye kwake kwa takribani miaka 19 sasa humpa taarifa juu ya kila mtu mbaya anayetaka kuja kwake na kumdhuru na ameweza kumnusuru dhidi ya majanga mbalimbali. "akipata taarifa huko ananipa mimi, kunakitu ambacho kiko mwilini mwangu kama kunatatizo huku sehemu ile inaanza kutikisika"

Vyakula vya Mbuzi huyo anapendelea zaidi kula nyama za kuku na hata nyama za mbuzi wenzake, pia anakula maandazi, na anapendelea kunywa chai. Bw Antony anasema kuwa mbuzi huyo anauwezo wa kufungua bomba mwenyewe na kunywa maji

chanzo BBC