Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:50 am

NEWS: MEYA WA UBUNGO AKANUSHA VIKALI TAARIFA ZA KUHAMIA CCM

Dar es salaam: Meya wa Manispaa ya Ubungo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Boniface Jacob amewatoa hofu wanachama na wadau wa chama hicho baada ya kusema kuwa hayuko tayari kukihama chama hicho na na kusema watu wanaozusha taarifa za yeye kukihama chama hicho ni uzushi na amewataka waache kuota ndoto zisizo wezekana.

Kupitia ukurasa wake 'twitter' Jacob amesema kuwa hayuko tayari kufanya hivyo na yuko tayari kukipigania chama chake hadi kifo chake.

"Waambieni wanaotamani nihamie CCM, nipo tayari kufa nikipigania chama changu CHADEMA na Sipo tayari kuwa takataka kwa kuhamia CCM!, iwe kwa pesa vitisho au kifo acheni kuota ndoto zisizowezekana", amesema Jacob.

Zimekuwepo taarifa za hivi karibuni zinazomuhusisha Moja kwa moja Meya huyo kutimkia Chama cha Mapinduzi CCM taarifa ambazo amekuwa akikanusha kila kukicha.

hadi sasa wabunge saba wa upinzani wamevihama vyama vyao na kujiunga na CCM, akiwemo mbunge wa Simanjiro (Chadema), James Ole Millya aliyejiunga CCM leo.

Wabunge hao ni Maulid Mtulia (Kinondoni), Dk Godwin Mollel (Siha), Julius Kalanga (Monduli), Mwita Waitara (Ukonga). Wanne hao walipojiunga CCM walipitishwa kuwania ubunge na kuibuka na ushindi.

Wengine ni Zuberi Kuchauka (Liwale) ambaye pia amepitishwa na CCM kuwania ubunge katika jimbo hilo kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 13, 2018. Mwingine ni Marwa Chacha aliyekuwa mbunge wa Serengeti kwa tiketi ya Chadema.

Juzi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema kuwa wabunge wa upinzani wanaotaka kujiunga na chama hicho tawala mwisho wa kufanya hivyo ni Desemba, 2018.

Polepole amesema mwaka 2018 ndio mwisho wa chaguzi ndogo za ubunge, wale watakaoshindwa kuhamia CCM wabaki walipo.

Imeandikwa na Deyssa H. Issa

Na kuhaririwa na Omary Swaudin

Muakilishi Publisher