- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MENEJA WA DIAMOND PLATNUMZ BABU TALE AKAMATWA NA JESHI LA POLISI
Dar es Salaam: Meneja mkuu wa star nguli wa Muziki nchini Tanzania Diamond Platnumz Hamisi Taletale maarufu Babu Tale, amekamatwa na jeshi la polisi Kanda Maalum Dar es Salaam na kufikishwa mahakamani kwa amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Meneja huyo amekamatwa Leo May 22 kupitia amri ya mahakama ya February 16 mwaka huu na Naibu msajili wa mahakama kuu kanda maalum ya Dar es salaam Wilbard mashauri alipo elekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale.
Amri hiyo pia, ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine. Hata hivyo, Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama hiyo ikatoa amri nyingine kama hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa wakitafutwa bila mafanikio hadi jana alipokamatwa.
Mahakama hiyo iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh250 milioni, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki. Baada ya kutiwa mbaroni leo alifikishwa mahakamani saa tisa alasiri kwa ajili ya hatua zaidi. Hata hivyo, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, aliyetoa amri ya kumkamata hakuwepo.
Kufuatia kutokuwepo kwa msajili huyo Taletale amerudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi hadi kesho asubuhi atakapopelekwa tena mahakamani hapo kwa hatua zaidi. Hukumu hiyo iliyomwamuru Babu Tale na nduguye kulipa kiasi hicho cha fedha, ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18,2016 katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde kutokana akiwalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.