- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MELI YAZAMISHA ZAIDI YA WATU 50 NCHINI CONGO
Taarifa kutoka nchini Congo zinasema kuwa Maiti zaidi ya 50 zimetolewa kwenye maji baada ya meli moja kuzama juzi Jumatano katika mto mmoja kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa takwimu za serikali.
"Ajali hii ilitokea usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, tuligundua miili 49 siku ya Alhamisi na mwili mwingine umeonekana Ijumaa hii asubuhi," Richard Mboyo Iluka, naibu gavana wa jimbo la Tshuapa (magharibi) ameliambia shirika la habari la AFP.
Ajali hiyo ilitokea kwenye mto Momboyo katika eneo la Monkoto, kilomita 750 kutoka Mbandaka, mji mkuu wa mkoa jirani wa Equateur.
Meli hiyo ya mtu binafsi ilikuwa ikifanya safari ya Mbandaka-Monkoto, huku ikiwa na abiria zaidi ya 50 na kiasi kikubwa cha bidhaa, kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na AFP.
"Sababu za ajali hiyo na idadi ya watu ambao hawajapatikana haijajulikana. Ujumbe kutoka kwa serikali ya mkoa huo tayari umetumwa katika eeneo la tukio kujua hali halisi ya mambo," Bw Mboyo ameongeza.
Ajali kama hii zinatokea mara kwa mara nchini DRC, kwenye maziwa au kwenye mito, na ajali hizi mara nyingi zimekua zikisababisha vifo vya watu wengi.
Mnamo mwezi Februari, watu zaidi ya kumi na nne walikosekana katika ajali ya meli mbeli zilizozama katika Mto Congo.