- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MCHUNGAJI AFUNGUKA KUHUSU WAUMINI KUCHATI SANA.
DOM: Imeelezwa kuwa baadhi ya waumini wa dini ya kikiristo hutumia muda mwingi kuchati na kuangalia picha zisizokuwa na maadili kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp kuliko kusoma maandiko matakatifu (Biblie} pindi wawapo majumbani.
Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki hii na Askofu wa kanisa la Uamsho la agano jipya la Tanzania lililopo Mbwanga jijini Dodoma Jackson Leguna wakati wa ibada ya kuwatengemeza wachungaji wa makanisa yote kitaifa iliyofanyika kanisani hapo.
Askofu Leguna amesema waumini wengi wamekuwa wakitumia simu zao kuchati mambo ambayo yanazungumzia habari za ngono na si kutumia kwaajili ya kuongelea utukufu wa Mungu.
Mbali na hayo Askofu huyo amewataka watanzania kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa kazi anazofanya na kuongeza kwa kusema kama Rais ataombewa amani iliyopo itazidi kupenya kila kona.