Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:39 am

NEWS: MCHUMBA WA KHASHOGGI AKATAA MWALIKO WA TRUMP KWENDA IKULU

Hatice Cengiz Mchumba wa mwanahabari wa Saudia aliyeuawa ndani ya Ubalozi mdogo wa Saudia nchini Uturuki Jamal Khashoggi anasema amesusia mwaliko wa rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwasababu Rais huyo wa Marekeni haijaonesha nia ya dhati kutaka kujua ukweli kuhusu mauaji hayo ya kikatili.

Hatice Cengiz amekiambia kituo kimoja cha Televisheni nchini Uturuki kwamba mwaliko huo unalenga kubadili maoni ya Wamarekani juu ya kifo hicho.

Riyadh imekanusha madai ya kuhusishwa kwa familia ya kifalme katika mauaji hayo na badala yake imelaumu watu iliyowataja kuwa''maajenti wakatili'

Katika mahojiano ya kusikitisha katika televisheni bi Cengiz alielezea jinsi mchumba wake alivyotoweka baada ya kuingia ubalozi wa Saudia mjini Istanbul.

Anasema ''Kama ningelijua maajenti wa Saudia walikua na njama ya kumuangamiza singelimruhusu kuingia humo''

Awali Saudia ilidai kuwa mwanahabari huyo ambaye alikuwa akiishi Marekani alitoka ndani ya ubalozi wake.

Baada ya shinikizo wakasema kuwa aliuawa alipojaribu kupambana na baadaye wakakiri kuwa aliuawa katika opersheni isiyo rasmi na ambayo haikubarikiwa na Bin Salman.