- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MCHINA ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUMPA RUSHWA RC
Geita: Mtu mmoja Raia wa China amefikishwa mahakamani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kwa kosa la mkupa Rushwa ya Tsh. Milioni 1 Mkuu wa mkoa wa Geita Bw. Robert Gabriel.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Desemba 7, 2018 na Mkuu wa taasisi hiyo mkoani Geita, Thobias Ndaro inasema mshtakiwa huyo, Cheng Li ni mfanyabiashara wa madini.
Mchina huyo alifikishwa mahakamani jana Novemba 6, 2018 mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Jovith Kato.
Akisoma mashtaka mwendesha mashtaka wa Takukuru, Dennis Lekayo amedai mahakamani hapo kuwa Oktoba na Novemba, 2018 mshtakiwa alimshawishi Gabriel kwa njia ya ujumbe wa simu akitaka kumpatia Sh1milioni kila mwezi.
Ilielezwa mahakamani hapo kuwa katika kuonyesha amedhamiria kutoa rushwa alituma ujumbe mwingine akimshawishi kumpelekea kiasi hicho cha fedha na majani ya chai kutoka China.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya ujumbe huo, mkuu huyo wa mkoa alitoa taarifa Takukuru ambao waliweka mtego uliofanikisha kumkamata mshtakiwa akiwa ofisini kwa Gabriel akijiandaa kutoa rushwa ya Sh1milioni na majani hayo ya chai.
Mshtakiwa amekwama makosa na yuko nje kwa dhamana huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Desemba 20, 2018.