- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MCHAKATO WA KUANZISHA MAMALAKA YA HIFADHI ZA FUKWE WAIVA
MTWARA: Wizara ya Maliasili na Utalii imesema ipo mbioni kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi za Fukwe nchini ili ziweze kusimamiwa ipasavyo kwa kujenga miundombinu bora itakayowavutia watalii wengi na hatimaye kuongeza pato la taifa.
Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa alipokuwa anawasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amebainisha hayo wakati alipotembelea Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano wa Mto Ruvuma katika wilaya ya Mtwara vijijini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara ya kubainisha vivutio vya Utalii vilivyopo mikoa ya Kusini.
Amesema Tanzania imejaliwa kuwa na fukwe nzuri lakini fukwe hizo zimekuwa zikitumika visivyo baadala ya kutumika kama chanzo cha mapato kupitia watalii.
Amefafanu kuwa fukwe zilizo nyingi zipo tu na zimekuwa hazina uwekezaji wa namna yeyote ile wakati ni rasilimali muhimu sana katika kuongeza pato la taifa kwa vile watalii walio wengi kwa sasawameanza kuugeukia utalii fukwe baadala ya wanyamapori.
Akizungumzia hatua za awali ambazo Wizara inazifanya kwa sasa, Naibu Waziri huyo amesema wameshaanza mazungumzo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambayo ndio Wizara inayozisimamia fukwe hizo kwa sasa.
Kwa upande wake, Kaimu Mhifadhi Mfawidhi Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Muingiliano ya Mto Ruvuma, Jennifer Simbu amesema mchakato wa kuunda Mamlaka hiyo uharakishwe ili Hifadhi hizo ziweze kuongeza pato la taifa kwa vile zitakuwa na uwezo wa kujitangaza.
Aidha, Mhifadhi huyo Jennifer Simbu amesema mwaka 2010 kuna baadhi ya Wawekezaji walijitokeza wakitaka kuwekeza lakini hadi hivi sasa hakuna hata Mwekezaji hata mmoja kati ya watano waliopewa maeneo hakuna aliyeyaendeleza.