- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA UKEREWE AJIVUA UWANACHAMA CHADEMA NA KUJIUNGA NA CCM
Mwanza: Mbunge wa Ukerewe, Joseph Michael Mkundi ametangaza kujiuzulu uanachama na nyadhifa zake zote ndani ya cha cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, na kuomba kujiunga cha cha Mapinduzi CCM.
Mukundi ametoa sababu nyingi lakini Miongoni mwa sababu alizotoa, ni kutopata ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzake (CHADEMA) wakati wa ajali ya MV Nyerere.
"Chama cha Siasa kama Taasisi ya Umma na inayotoa maelekezo Kwetu wawakilishi wa Wananchi, yenyewe inapokuwa msingi wa Kujenga Chuki, uhasama, ubaguzi na Ukinzani na serikali. Taasisi hii inapoteza Uhalali wa Kiuongozi (leadershipLegitimacy).
"Kwa Msingi Huo Leo Siku ya Jumatano tarehe 10 Oktoba 2018 natangaza kujivua uanachama wa Chadema na hii ikiwa kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema ibara ya 5.4.1,chama ambacho kwa Tiketi yake nilikuwa Diwani wa Kata ya Bukiko na Mbunge wa Jimbo la Ukerewe
"Natangaza kuomba Kujiunga na CCM, Chama ambacho kwa hakika nimeona wakidhihirisha kwa Vitendo Itikadi yao ambayo imejengwa katika misingi ya Utu, Undugu, Mshikamano, Haki na Umoja wa watu wa Tanzania" -Joseph Michael Mkundi