Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 8:39 am

NEWS: MBUNGE WA CHADEMA UKONGA AJIUZULU NA KUJIUNGA NA CCM

Dar es salaam: Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikwabe Waitara, atangaza kujiuzulu CHADEMA na kuhamia CCM.

Kajiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Asema sababu ni kutofautiana na viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA baada ya kuhoji kuhusu matumzi ya Ruzuku pamoja na demokrasia ndani ya chama

Ameeleza kuwa alihoji matumizi ya Milioni 237 za ruzuku kwani mpaka sasa CHADEMA haina Ofisi Kuu, ya Kanda wala Mkoa

Mwenge wa Uhuru umekuja kuzindua miradi ya maendeleo niliyoipigania lakini naambiwa usiende pale na mimi shida yangu haikuwa CCM pale ilikuwa ni mradi niliopigania

"Leo nimejiondoa rasmi CHADEMA kwahiyo mimi sio Mbunge tena, nimetupa jongoo na mti wake" amesema Mwita Waitara

“Mimi nataka niende mahali ambako kuna kazi za kufanya,” Waitara amewaambia waandishi na kuongeza kwamba anatamani kuwa Waziri Kamili.

Waitara ametangaza uamuzi wake huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba mjini hapa, akiwa sambamba na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.

Kwa uamuzi huo wa Waitara ambaye alikuwa CCM kabla ya kujiunga Chadema, jimbo la Ukonga linabaki wazi.

Waitara amekuwa mbunge wa pili wa Chadema na wa tatu wa upinzani kuhama chama na kujiunga na CCM.

Wengine wa Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni).