Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 7:32 am

NEWS: MBUNGE MSINGWA ASUSIA JESHI LA POLISI.


Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa amegoma kutoa maelezo aliyotakiwa kutoa kwa Jeshi la Polisi baada ya kudaiwa kuwa ametamka maneno ya uchochezi katika mkutano wa hadhara alioufanya katika kata ya Kihesa Wikiendi iliyopita.

Akizungumza na www.eatv.tv, Msigwa amesema kuwa mapema asubuhi ya leo aliitwa Polisi na kushikiliwa kwa muda akitakiwa kutoa maelezo lakini hakufanya hivyo, suala lililopekea kutishiwa kuwekwa rumande.

"Nilishikiliwa na Polisi kwa muda nikitakiwa kutoa maelezo kwa kile walichodai kuwa nimetoa lugha ya uchochezi kwenye mkutano wa hadhara lakini sikufanya hivyo nimegoma na wakasema wataniita wakinihitaji tena", amesema Mch. Msigwa.

Mapema asubuhi ya leo Oktoba 9, Mkuu wa Polisi wilaya ya Iringa Yohana Mjengi alimwandikia barua mbunge huyo akimtaarifu kusitisha kibali alichopewa cha kufanya mikutano ya hadhara katika Wilaya hiyo kwa madai kuwa ametumia lugha ya uchochezi katika mkutano wake.