Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:33 am

NEWS: MBUNGE HECHE ASHANGAZWA NA KAULI YA RAIS NA WAZIRI KUPISHANA

Dodoma: Mbunge wa Tarime mjini John Heche amesema kuwa ameshindwa kuelewa kati ya kauli ya Rais Magufuli na Waziri wa maswala ya Fedha Dr. Philipo Mpango juu ya utata uliopo kutokana na kauli mbili kinzani juu ya Fedha za ujenzi wa Standard gauge Railway, akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram Heche amesema kuwa Rais Magufuli aliwahi kusema kuwa reli ya Standard gauge ( SGR) inajengwa kwa pesa za watanzania, wakati huo huo Waziri wa Fedha anasema kwenye Kitabu chake kuwa Ujenzi wa Reli ya SGR tumejenga kwa mkopo

''Rais aliwambia Watanzania reli ya SGR tunajenga kwa pesa zetu wenyewe leo waziri anasema kwenye kitabu chake kwamba ni mkopo Watanzania wamuamini nani?


''Kama kwa mwaka mmoja tu tunakopa 17% ya deni letu miaka mitatu kama trend itakua hivyo tutakua wapi? Na kwanini Watanzania hawaambiwi ukweli kwasababu mwisho wa siku wao ndio watalipa deni hilo. alisema Heche

Jana Waziri wa fedha nchini Dr. Philipo Mpango alisem a kuwa Deni la Taifa liliongezeka kufikia Dola za marekani milioni 26,115.2 kwa mwezi Juni 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 17% kutoka dola 22,320.76 kwa mwaka 2016.

Mpango alisema kuwa ongezeko la deni hilo ni kutokana na mikopo mipya iliyokokwapwa kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo kama vile Standard gauge Railway cities na Usafirishaji Dar es salaam DART


Imeandikwa na Deyssa h. Deyssa