Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:38 pm

NEWS: MBUNGE HECHE AMPA MAKAVU WAZARI MPANGO

Dodoma: Leo Jumatano Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kutoa maelezo sahihi Bungeni kuwa ni Watanzania wangapi wamewaondoa katika unyonge na umaskini tangu Serikali ya Rais Magufuli iingie madarakani.

“Mnajinasibu kuwa ni Serikali ya wanyonge, wanyonge ni nyie mnaoendesha maVX? Waziri Mpango utakapokuja kuhitimisha hoja yako mlikuta wanyonge wangapi? Mmepunguza wangapi?” Amehoji Heche

Heche ametoa kauli hiyo Dodoma bungeni leo Novemba 6, 2018 wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2019/20.

Amesema katika mwaka wa fedha 2017/18 Serikali ilitenga Sh12 trilioni lakini ilipeleka Sh 6 trilioni katika maendeleo.

“Mnasema mmekusanya fedha nyingi, ziko wapi? Mnazilalia? Kwa sababu kwa wananchi wala mtaani hazionekani,” amesema.

Heche amesema watu wanaosema ukweli wamekuwa wakitishiwa na kuwaundia makosa.

Heche alimsifu Mbunge wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe kwa juhudi anazofanya za kuikosoa serekali.

“Mheshimiwa Zito (Mbunge wa Kigoma Mjini-Zitto Kabwe) endelea hivyo hivyo. Wengine tunaishi kwa kuhama hama,” amesema.