- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE BWEGE NA WENZAKE WAACHILIWA KWA DHAMANA
Dar es Salaam: Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha Wananchi CUF, Seleman Bungara maarufu kama ‘bwege’ na viongozi wenzake wawili wameachiliwa kwa dhamana na Mahakama ya Mkoa wa Lindi.
Viongozi wengine waliachiliwa huru leo Ijumaa Novemba 23, 2018 ni pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa umma, Mbarara Maharagande na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Abuu Mjaka.
Kwamujibu wa Wakili wa washtakiwa, Rainery Songea amesema wateja wake wote walitakiwa watoke jana baada ya kupata dhamana hiyo lakini kukajitokeza hitilafu kwenye barua za wadhamani hali iliyosababisha warudishwe mahabusu.
“Leo kasoro hizo zimerekebishwa na wameachiliwa huru na kesi ya itatajwa tena Desemba 3 mwaka huu,”amesema Wakili Songea.
Viongozi hao walifikishwa jana mahakamani hapo wakikabiliwa na mashtaka ya kutishia, kutoa lugha isiyofaa na kushawishi watu kufanya makosa.