Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:41 pm

NEWS: MBUNGE AHOJI MPANGO WA SERIKALI KULETA BAADHI YA SHERIA ZILIZOPITWA NA WAKATI BUNGENI.

BUNGENI DOM: Wizara ya Sheria na Katika imesema katika kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinakidhi mahitaji ya wakati, Serikali imekuwa ikifanya mapitio ya sheria kupitia tume ya kurekebisha sheria Tanzania.


Ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Vijana,Anthony Mavunde wakati akijibu swali kwa niaba ya Wizara ya Sheria na Katiba.


Mavunde alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kavuu,Pudenciana Kikwembe (CCM) ambaye alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuleta baadhi ya sheria zilizopitwa na wakati bungeni ili ziweze kupitiwa upya ziendane na wakati hasa sheria za usalama barabarani.


Akijibu swali hilo,Mavunde amesema katika kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinakidhi mahitaji ya wakati Serikali imekuwa ikifanya mapitio ya sheria kupitia tume ya kurekebisha sheria Tanzania ambayo ipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.


Amesema hayo yamekuwa ikifanya mapitio na tafiti mbalimbali ambazo zimekuwa msingi wa marekebisho ya sheria ama kutungwa kwa sheria mpya hapa nchini.


“Kazi za mapitio ya sheria ni kazi endelevu na Serikali itaendelea kuwasilisha bungeni miswada ya sheria ambayo inalenga kurekebisha sheria za nchi au kutunga sheria mpya ili kukidhi matakwa ya wakati,”amesema Mavunde.