- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE NA MATIKO KULA KRISMASI SEGEREA
Dar es Salaam: Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mweka hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko itawalazimu kula siku kuu ya Krismasi Segerea kutokana na mahakama ya hakimu mkazi kisutu kuhairisha kesi yao hadi Januari 3, 2019
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Simon Wankyo akisaidia na wakili Salim Msemo amedai leo Ijumaa Desemba 21, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa tu .
Wakili Simon amedai kuwa hawana taarifa ya kinachoendelea mahakama ya juu hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo, wakili Faraja Mangula amedai kuwa wakili wa washitakiwa hao Peter Kibatala na Sheck Mfinanga wamepata dharura hivyo wanaomba mahakama ipange Januari 4, 2019.
Akijibu hoja hiyo, wakili Simon amedai wanaiachia mahakama ipange tarehe itakayoona inafaa na hakimu Mashauri kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 3, 2019.
Mbowe na Matiko wako gereza la Segerea baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana Novemba 23, 2018 kwa kukiuka masharti ya dhamana ikiwemo kutoka nje ya nchi bila kibali.
Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ya jinai namba 112/2018 ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicenti Mashinji; makatibu naibu wakuu, Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara).
Wengine ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Bunda, Mchungaji Peter Msigwa; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.
Mbowe na viongozi wengine wanakabiliwa na mashtaka 13 ya uchochezi, uasi na kuhamasisha wafuasi wao kutenda makosa, hakuweza kufika mahakamani wakati kesi yao ilipotajwa.