- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE AWASHUKIA WANAOHAMIA CCM, KUWA WAPO KIMASLAHI
Dar es salaam: Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe, amesema wabunge wanaokimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanafuata maslahi na kwamba wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu upinzani hauwezi kuwazuia kufanya hivyo.
Kauli ya Mbowe imetolewa ikiwa siku moja tangu kutolewa taarifa katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM kuwa kuna mbunge na madiwani wanane kutoka upinzani ambao wanamwomba Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli, kuhamia CCM.
Mbowe alipoulizwa kuhusu msimamo wa upinzani dhidi ya wimbi la wabunge wa upinzani kukimbilia CCM, Mbowe alisema “Mtu kama hakusaidii ana faida gani na wewe?...waache wahame, mtu anapokulilia shida na wewe unakuwa msikivu, anaponunuliwa mwache aende, si walikuwa huko huko, waache aende wanafahamu siri za kwao.”
Ameongeza kwamba “Wao kwa sababu wameshikilia kila kitu waache wafanye wanavyotaka. Hatumzuii mtu kuhama chama, anahama chama anakwenda kwenye maslahi,”.
Aidha, Mbowe ameongeza kwamba "CCM walisema ifikapo mwaka 2020 upinzani hautakuwapo, hivyo wanafanya hivyo kutimiza ndoto yao. Lakini ngoja nikuambie, upinzani tutaendelea kuwapo na tutaendelea zaidi kuwapo. Serikali bila upinzani haiwezi kuitwa serikali, ndiyo maana ya demokrasia. Hata Kenya hawajasimamia sehemu moja. Ifikapo sehemu fulani tutamwapisha mtu fulani,”.
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alidai kuwa wao (CCM) wanatumia fedha, lakini upinzani wanatumia nguvu kutetea wananchi.
Hamahama ya wabunge ilianza Oktoba 30, mwaka huu, baada ya Lazaro Nyalandu (45), aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki tangu mwaka 2000, kujiuzulu kwa madai ya kukosekana kwa demokrasia ya kutosha ndani ya CCM.
Mapema wiki hii kwenye Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Rais Magufuli alisema kwa sasa kuna watu wengi wanaorejea CCM kutoka upinzani na wengine wanaojiunga na chama hicho kwa mara ya kwanza na kwamba yupo mbunge ambaye anamuomba sana kuhamia CCM akiwa na madiwani nane