- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE ATOA POVU SAKATA LA KUPIGWA RISASI KWA TUNDU LISSU
DODOMA: Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Hai Freeman Mbowe amefunguka nakuitaka serikali kuviruhusu vyombo vyakimataifa kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la kupigwa risasi kwa mbunge wa singida mashariki Tundu lissu.
Akiuliza swalikwa waziri mkuu Kassimu Majaliwa leo bungeni mjini Dodoma leo Mbowe alitaka kujua mpango wa serikali wa kuthibiti matukio ya kupigwa risasi,kuonewa na kupotea kwa baadhi ya viongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Mbowe amesema usalama wa nchina mahusiano mema miongoni mwaraia ni tunda la mahusiano mazuri kati ya vyama vya siasa, serikali na vyombo vya dola huku akisema,tukio la kushambuliwa kwa Lissu limezua sintofahamu na hofu kwa wananchi pamoja na mataifa ya kigeni.
Akijibu swali hilo waziri mkuu kassim Majaliwaamesema amani nautulivu ndani ya nchini lazima watanzania na jamii nzima kuwana ushirikiano ili kulinda heshima ya taifa la Tanzania .
Aidha amesema vyombo vya dola nchini vinaendelea kufanya uchunguzi mpaka utakapokamili vitakuja kutoa taarifa kamili na zenye uhakika.
‘’Nataka kukuhakikishia kuwa vyombo Vya dola havijakaa kimya na vinaendelea kufanya uchunguzi wa suala hilo,’’amesema.
Waziri huyo amewasihi wanafamilia na watanzania kiujumla kuendelea kuwa watulivu na kujenga imani mpaka uchunguzi utakapokamilika.
Mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu alipigwa risasi septemba 7 nyumbani kwake mjini Dodoma wakati wa vikao vya bunge vikiendelea.EWS