- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBARONI KWA KUJIFANYA KATIBU MKUU WA IKULU DAR
Dar es salaam: Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linamshikilia mwanaume mmoja Seif Abdallah Mohamed Mkazi wa Tuangoma Kigamboni jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kujifanya Katibu Mkuu kiongozi wa Ikulu na kuendesha vitendo vya Utapeli katika ofisi mbalimbali za serikali ikiwemo wizara ya mambo ya ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Octoba 26, 2018 Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas amesema Seif mwenye Umri wa miaka thelathini na mitano alitiwa mbaroni baada ya kumpigia simu kiongozi mmoja wa ngazi ya juu, kwa nia ya kutekeleza vitendo hivyo vya Utapeli.
Kamanda Sabas amesema Seif anatuhumiwa kuwa amekuwa akitumia majina zaidi ya manne katika vitendo hivyo vya utapeli ikiwemo kujitambulisha kama mkuu wa nidhamu na maadili wa chama cha mapinduzi.