- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBABE WA KIVITA CONGO BW. BEMBA ASEMA UCHAGUZI WA CONGO NI MZAHA
DRC: Jean Pierre Bemba Jumanne ambaye aliyekuwa mbabe wa kivita nchini DRC amedai kuwa uchaguzi uliocheleweshwa utakaofanyika Desemba nchini humo ni mzaha tu baada ya mahakama ya katiba kumnyima nafasi ya kuwania urais.
Bemba ni miongoni mwa wagombea 6 walioondolewa kwenye orodha ya kugombania urais na tume ya uchaguzi kwenye zoezi hilo lililopangwa kufanyika decemba 23.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wakati akifanya mahojiano na televisheni ya France 24, Bemba alisema ni jambo la kuhuzunisha kumuona rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akimtu akichagua ni nani watakaokuwa wapinzani wake.
Rais Joseph Kabila ambaye ametawala taifa hilo tangu 2001 hatimaye ametangaza kutowania urais kwa muhula mwingine baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.
Hali ya taharuki na ghasia imeendelea kushuhudiwa kote nchini humo. Taifa hilo lililokuwa chini ya ukoloni wa Ubelgiji halijashuhudia mabadilishano ya amani ya madaraka tangu lilipojipatia uhuru mwaka wa 1960.