- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MATUMIZI MABAYA YA CHAKULA KIPINDI CHA JANDO LAWATIKISA MADIWANI
BAHI DOM: Wakazi wa wilaya ya Bahi mkoani Dodoma wamekuwa wakitumia vibaya chakula wakati wa tohara za watoto wa kiume(jando)hali inayosababisha kukumbwa na njaa.
Wakizungumza katika kikao cha baraza la madiwani cha halmashauri hiyo,Diwani wa Mtitaa Jamaly Shabiby amesema kuwa suala la matumizi mabaya ya mazao msimu wa jando limekuwa ni tatizo kubwa ambalo linasababisha upungufu wa chakula.
“Hakuna kitu ambacho kinaudhi kama unapofika msimu wa mavuno baada ya watoto kufunga shule, basi wananchi wetu wanatumia mazao waliyopata kwenye majando na wengine kupikia pombe, hichi kipindi ndicho ambacho watu wetu hawa wanatumia ovyo chakula,”amesema.
Akiendelea kuelezea amesemajando huchukua takriban mwezi mmoja hali ambayo chakula kingi hupikwa pamoja na pombe za kienyeji.
Naye, Diwani wa kata ya Mpinga Gaitan Muyinga amesema ni vyema ikatungwa sheria ndogo ambayo itapunguza matumizi mabaya ya chakula.
“Hapa tuweke sheria ndogo badala ya wazazi kujenga nyumba maalum kwa ajili ya majando sasa, wawaweke watoto ndani ya nyumba zao na bila kuwa na sherehe ili kuondokana na matumizi makubwa ya chakula msimu huu, hatukatazi mila na desturi lakini tuangalie tunakoelekea sasa,”amesema.
Kwa upande wake, Diwani wa Babayu Hussein Kamau amesema kuna mwamko mdogo wa wananchi kuchangia miradi ya maendeleo huku akishauri waelimishwe kuondokana na sherehe zisizo za msingi .
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Sostenes Mpandu amesema suala hilo si la kupuuzwa pamoja na kwamba wanaenzi mila na desturi na kwamba ni vyema elimu ikatolewa ili kuondokana na matumizi ovyo ya chakula msimu huo.
Naye Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Rachel Chuwa amesema kuna mikoa mingine imefanikiwa kuondokana na masuala ya unyago ambayo hutumia muda na chakula kingi baada ya kupatiwa elimu.
“Yaani kwa wananchi wetu kipindi cha likizo ya mwezi wa sita hapa kulikuwa na ngoma nyingi za majando na kweli haya majando yanachukua muda mrefu na chakula kingi, matokeo yake yakiisha wanaanza kulalamika njaa,”amesema