- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MASHINDANO YA DODOMA HALF MARATHON KUFANYIKA MWEZI NOVEMBER.
DODOMA: Mashindano ya riadha ya mbio ndefu ya Dodoma half Marathon yanataraji kufanyika mkoani Dodoma huku lengo likiwa ni kukuza mchezo wa riadha kanda ya kati na kuibua vipaji vya wanariadha wapya watakaoweza kupeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma mkurugenzi wa Vision Sport ambao ndio waratibu wa mashindano hayo Ally Nchanga amesema kuwa lengo lao ni kuona riadha kanda ya kati inakuwa kwa kasi kubwa.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan RugimbanA amesema mkoa wake uko tayari kushiriki mashindano hayo na kudai kuwa mashindano hayo yatawezesha kupata wachezaji wazuri na wenye vipaji.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya tigo ambapo Kaimu Mkurugenzi wa tigo Kanda Henry Kinabo amesema wametoa mil 20 kama mwanzo tu lakini wataendelea kuwa pamoja katika mashindano hayo.
Mashindano ya Riadha yam bio Ndefu yanataraji kuanza Mapem,a Nov 12 mwaka huu ambapo zawadi kwa washindi zitskuwa fedha na medali