Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 8:45 am

NEWS : MASHAMBULIZI DHIDI YA MAENEO YA MAGAIDI YAENDELEA NCHINI LIBYA

Jeshi la taifa la Libya limetangaza kuwa, limeshambulia maficho kadhaa ya magaidi katika mji wa Derna wa mashariki mwa nchi hiyo.

Katika taarifa yake iliyoitoa jana (Jumapili) jeshi la taifa la Libya limesema, mbali na kushambulia maficho ya magaidi katika mji wa Derna, askari wa jeshi hilo wameandaa kivuko maalumu cha kuhakikisha kuwa raia wa kawaida wanatoka salama mjini humo.

Tarehe 7 mwezi huu wa Mei jeshi hilo la Libya linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar lilianzisha operesheni kubwa ya kuukomboa mji wa Derna kutoka mikononi mwa magaidi

Image result for libya explosion

Kwa muda mrefu sasa mji wa Derna wa mashariki mwa Libya unadhibitiwa na kundi la kigaidi linalojiita Baraza la Mujahid wa Derna, ambalo ni moja ya matawi ya mtandao ya kigaidi wa al Qaida huko nchini Libya.

Libya ilitumbukia kwenye machafuko tangu mwaka 2011 wakati wa kampeni za kuung'oa madarakani utawala wa Kanali Muammar Gaddafi.

Marekani na nchi za Magharibi ziliivamia kijeshi nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, zikafanya uharibifu wa kupindukia kwenye miundombinu ya nchi hiyo na baadaye kuitelekeza nchi huku silaha zikiwa zimezagaa mikononi mwa makundi hasimu.

Tangu wakati huo hadi leo hii Libya haijawahi kushuhudia utilivu hata siku moja kutokana na kila kundi kuendelea kupigania nafasi kubwa zaidi nchini humo