Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:51 am

NEWS: MASAUNI: SERIKALI HAIKUSUDI KUFUTA TOZO KINGA ZIDI YA MOTO

DODOMA:Jeshi la zimamoto na ukoaji inawaasa wananchi kujenga nyumba zao kwa kufuata sheria za kanuni zinazosimamia mipango mijiili kuwa na miji salama na kupunguza athari zitokanazo na moto na majanga mbalimbali.

Akijibu swali la bunge wa mpanda mjini Sabastian Kapufi aliyetaka kujua ‘ je, serikali ina mpango gani wa kufuta ada ya malipo ya sh 150000 kwa ajili ya kodi ya zimamoto pale wanapotaka kupimiwa ili kupunguza ongezeko la makazi holela’.

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Masauni Amesema jeshi la zimamoto na uokoaji linafanya ukaguzi kwa mujibu wa sheria namba 14 sura na. 427 ya mwaka 2007 kupitia kanuni zake za ukaguzi na vyeti 2008 ikisomwa pamoja nay a mwaka 2014 (fire and Rescue force (safety Insepections, certificates anda fire levy) Regulations, 2008 na 2014.

Amesema kwa mujibu wa kanuni za ukaguzi za mwaka 2014 (Fire levy category Na. 58) kanuni inaelekeza kutozwa tozo za usomaji na ushauri wa michoro au ramani za majengo.

Aidha kwa mujibu wa kanuni ya majengo ya mwaka 2015 yaani (The fire and rescue force ,(fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015 2015 na (248).

Mbali na hayo amesema kwa kuzingatia tahadhari na kinga dhidi ya moto, serikali haikusudii kufuta tozo hiyo kwa sasa.