Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:28 am

NEWS: MAREKANI YATUMA WANAJESHI 5,200 KUZUIA WAHAMIAJI MPAKA WA MEXICO

Serekali ya Marekani chini ya Utawala wa Donald Trump inawatuma wanajeshi 5,200 kwenda kusaidia kulinda mipaka kati ya nchi hiyo na Mexico, baada ya maelfu ya wahamiaji kutoka mataifa ya Amerika ya Kati kujiunga na msafara wa wahamiaji wanaopania kufika Marekani.

Idadi hiyo ya wanajeshi wanaotumwa kuulinda mpaka ni kubwa kuliko ilivyotarajiwa huku Rais Donald Trump akizidi kuwa na misimamo mikali kuhusu uhamiaji kuelekea chaguzi za kati kati ya muhula zinazotarajiwa tarehe 6 mwezi ujao wa Novemba.

Jenerali Terrrence O' Shaughnessy, anayesimamia kambi ya wanajeshi walioko Kaskazini mwa Marekani amesema wanajeshi 800 tayari wako njiani kueleka katika mpaka wa Texas na wengine wanaelekea katika mipaka ya California na Arizona. O'Shaugnessy amesema Rais Trump ameweka wazi kuwa ulinzi wa mipaka ni jambo la usalama wa kitaifa.

Huku hayo yakijiri, mamia ya wahamiaji kutoka Honduras wamevuka mto kuingia Mexico, hilo likiwa kundi jipya la wahamiaji wanaoelekea Marekani. Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya wahamiaji 7,000 wako njiani kuelekea Marekani.