Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:53 pm

NEWS: MAREKANI YATISHIA KUIWEKEA VIKWAZA MAHAKAMA YA ICC

Washington: Serekali ya Marekani imetishia kuiwekea vikwazo mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kama tu itaendeleza mipango yake ya kuwashtaki raia wa Marekani kwa madai ya kuwatesa wafungwa nchini Afghanistan.

Related image

Mahakama hiyo kwa sasa inatathmini kuwafungulia mashtaka wanajeshi wa Marekani

Mshauri wa masuala ya usalama ya kitaifa John Bolton alisema mahakama hiyo sio halali na kuapa kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuwalinda raia wake.

Image result for america against icc

Mahakama hiyo inachunguza na kuwaleta kwenye hukumu wale wanaohusika kwenye uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiingilia kati wakati mahakama za nchi haziwezi kuwahukumu.

ICC ilibuniwa chini ya mkataba wa Roma wa mwaka 2002 na imeungwa mkono na nchi 123 ikiwemo Uingereza.

Baadhi ya nchi za Afrika zimataja kuondoka kutoka mahakama hiyo zikisema kuwa inazionea nchi za Afrika.