Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:51 am

NEWS: MAREKANI YATAKA TENA MAZUNGUMZO NA KOREA KASKAZINI

Serekali ya Marekani kupitia Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mike Pompeo alisema siku ya Jumapili kwamba ndani ya wiki hii atafanya tena mazungumzo na afisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini Kim Yong Chol mjini New York.

Pompeo alisema mkutano huo utakuwa ni kuhusu mchakato wa juhudi za kusitisha silaha za nuklia za Korea Kaskazini.

Tangu Rais Donald Trump akutane na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UN nchini Singapore mwezi Juni, mpango wa kusitisha program ya nuklia ya nchi hiyo ya Peninsula ya Kore umeoneka kusuasua.

Pompeo alisema mazungumzo yajayo yatatoa fursa nzuri ya kupiga hatua ya kuridhisha kuhusu ratiba kamili ya ni lini Korea Kaskazini itakuwa imekamilisha mpango wake wa kuachana na programu yake ya silaha za nuklia.