Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:40 am

NEWS: MAREKANI YALAANI KITENDO CHA ODINGA KUJIONDOA KWENYE UCHAGUZI

Washington: Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imetoa taarifa yake kuwa inaheshimu maamuzi lakini inajutia uamuzi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, kujiondoa kwenye Uchaguzi mpya wa urais tarehe 26 mwezi huu.

Licha ya hayo Marekani imeendelea kusisitiza kuwa, itaendelea kushinikiza kuwepo kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.

Afisa wa juu katika Wizara hiyo ameliambia Gazeti la Daily Nation kuwa, pamoja na hilo Odinga anakaribishwa nchini Marekani.

Taarifa hii imekuja baada ya kuwepo kwa madai kuwa Odinga amenyimwa Visa ya kwenda Marekani.

Marekani imesema hakuna kinachomzuia Odinga kuja nchini Marekani wakati wowote anaotaka.

Kwa sasa Odinga yupo jijini London nchini Uingereza, anakotoa midhahara ya kisiasa na kukutana na viongozi mbalimbali.

Kenya imeendelea kugubikwa na maswala ya kisiasa tangu kufanyika kwa uchaguzi 8 Agosti mwaka huu amabapo katika uchaguzi huo Rais wa sasa Uhuru Kenyatta alitangazwa na tuma ya uchaguzi nchini humo IEBC kuwa ndiye mshindi, matokeo ambayo yalifutiliwa mbali na mahakama ya Juu nchini humo nakuagiza uchaguzi kurudiwa.