- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : MAREKANI YAKIRI HAIWEZI KUISHAMBULIA IRAN
'Marekani inakiri kuwa haiwezi kuishambulia kijeshi Iran'
Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran amesema: "Hali ya sasa ya nguvu za Iran na busara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, iko kwa namna ambayo, Marekani pamoja na vibaraka wake katika eneo wanakiri kuwa haiwezekani kuishambulia Iran kijeshi."
Meja Jenerali Mohammad Baqeri, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran ameyasema hayo leo Jumanne katika Kongamano la Usalama na Ulinzi wa Kaskazini Magharibi mwa Iran ambalo limefanyika katika mji wa Ourmieh. Ameongeza kuwa, njama za madola ya kibeberu dhidi ya Iran ya Kiislamu zilifeli tokea mwanzo na kwamba njama zote ambazo zinatekelezwa na Marekani hazitafanikiwa hata chembe.
Meja Jenerali Baqeri, ameashiria kupata pigo baada ya jingine magaidi wakufurishaji huko Iraq na Syria na kuongeza kuwa: "Kufuatia muongozo wa busara wa marajii wa kidini, serikali na jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq na Syria, leo magaidi wanakaribia kuangamizwa kikamilifu.
Wakati huo huo Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC Meja Jenerali Ali Jafari amesema leo kunasikika sauti ya kufeli na kusambaratika ubeberu na uistikbari wa kimataifa na kwa msingi huo Iran inapaswa kujiimarisha zaidi.
Meja Jenerali Jafari ameyasema hayo leo katika kongamano la 'Ulimwengu Usio na Ugaidi' ambalo limefanyika mjini Tehran na kuongeza kuwa: "Ulimwengu usio na ugaidi, usio na uistikbari na mfumo wa kibeberu ni ulimwengu unaoweza kufikiwa."
Kamanda wa IRGC amesema kila mara Marekani inapozidisha vikwazo, azma na irada ya Iran ya kuongeza nguvu zake za kujihami huimarika zaidi.
Meja Jenerali Jafari ameongeza kuwa, Marekani ndiye muungaji mkono mkubwa zaidi wa ugaidi na kubaini kuwa Washington pia ndiye muungaji mkono tawala bandia na ghasibu duniani.
Hali kadhalika amesema makombora ya Iran yenye uwezo wa kulenga shabaha umbali wa kilomita 2000 yanatosha kushambulia majeshi ya Marekani katika eneo iwapo Marekani itathubutu kuishambulia Iran