- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAMLAKA YA ANGA TANZANIA YAKANUSHA KUZUIA NDEGE YA FASTJET
Dar es Salaam: Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) limesema hawajamzui Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania Lawrence Masha kuingiza ndege zake Desemba 22, 2018 kama ilivyopangwa na shirika hilo, ikisisitiza kuwa usafiri wa anga haufanywi kwa ujanja.
Imesema kilichotokea ni kwamba maombi ya uingizaji wa ndege hizo yaliwasilishwa Desemba 24, 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 27, 2018 mkurugenzi mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema tangu shirika hilo lipewe notisi ya kusudio ya kufutiwa leseni Desemba 17, 2018, liliwasilisha andiko lake Desemba 24, 2018 na sasa bado mamlaka hiyo inalifanyia kazi.
"Madeni ya fastjet yalikuwa zaidi ya Sh6 bilioni ambazo wanadaiwa na watu tofauti, tayari wamelipa sehemu ya fedha wanazodaiwa na TCAA japo si zote. Usafiri wa ndege una masharti ya msingi ambayo yasipofuatwa ni hatari," amesema Johari.
“Miongoni mwa mambo ya msingi ni uwezo wa kifedha katika shirika, usafiri wa anga hakuna ujanja kama hatakidhi masharti leseni itafutwa tukisema tuhurumiane ni hatari tutaua watu, usafiri wa anga usiposimamiwa vizuri ni hatari kwa usalama utaua watu."
Jana Masha alisema Serikali haimpi ushirikiano wa kutosha katika mkakati wake wa kulifufua Shirika la Fastjet.
Huku akiongezea kuwa wamemzuia kuingiza ndege aina ya Boeing 737-500 baada ya iliyokuwepo kuzuiliwa kuruka kwa madai kuwa inapata hitilafu mara kwa mara na shirika halina meneja mwajibikaji.
Masha ametoa kauli hiyo wakati akifanyiwa mazungumzo na Shirika la Habari la MCL Digital na kubainisha kuwa ana matumaini kuwa baada ya kumalizika kwa sikukuu ya Krismasi huenda mambo yakawa mazuri.
Alisema ikiwa ataruhusiwa ndege hiyo itafika Tanzania ndani ya muda mfupi kwa maelezo kuwa kila kitu kipo tayari, “safari kutoka Afrika Kusini ilipo hiyo ndege hadi Tanzania ni mwendo wa masaa matatu tu.”
Alisema ndege iliyozuiwa ilikuwa imelipiwa tayari kwa kuruka ikiwa na wafanyakazi wote, hivyo kitendo cha kuizuia ni hasara.