Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 4:49 am

NEWS : MAMILIONI WAMIMINIKA KATIKA MAOMBOLEZO YA KARBALA ARUBAINI YA HUSSEIN

Mamilioni waendelea kuomboleza Karbala katika Arubaini ya Hussein (as)

Mamilioni waendelea kuomboleza Karbala katika Arubaini ya Hussein (as)

Mamilioni ya waumini wameendelea kuomboleza na kuzuru kaburi la mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (as) katika mji mtakatifu wa Karbala katika shughuli ya siku ya Arubaini ya mtukufu huyo.

Umati mkubwa wa watu ambao wengi wamewasili Karbala baada ya kutembea kwa miguu masafa ya kulomita karibu 80 kutoka katika mji wa Najaf, wanashiriki katika shughuli hiyo inayotambuliwa kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi wa kidini duniani.

Mahema yanaonekana kote katika barabara za kuelekea Karbala huku makundi ya watu wa kujitolea yakitoa huduma za chakula, maji na tiba bure kwa mamilioni ya watu wanaoeleka au waliowasili katika mji huo mtakatifu.

Shughuli ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume na masahaba zake wema ambao walisabilia roho zao wakipambana na mtawala dhalimu Yazid bin Muawiya kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika ardhi ya Karbala nchini Iraq.

Mamilioni ya Wairani wanashiriki katika shughuli ya Arubaini ya mwaka huu sambamba na mamilioni ya Waislamu kutoka maeneo mengine ya dunia. Msemaji wa Kamati ya Arubaini ya Iran, Shahriar Heidari, amesema Wairani 2.3 walikuwa wamewasili Iraq siku kadhaa zilizopita na kwamba idadi nyingine ya Wairani wapenzi wa Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw) ilitarajiwa kufika Karbala hususan leo Ijumaa.

Serikali ya Iraq imezidisha usalama na ulinzi kandokando ya mji wa Karbala ambako inapatikana Haram na kaburi la mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Hussein (as).