- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ''MAMBO MENGI TUNASHINDWA KUYASHUGHULIKIA KWA SABABU YA UKINZANI WA MILA'' KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA.
DOM: Katibu Mkuu Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dk Mpoki Ulisubisya amesema wanashindwa kushughulikia mambo mengine ikiwemo huduma za afya kwenye ngazi ya jamii kutokana na ukinzani wa mila na desturi zilizopo katika jamii.
Akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau cha kujadili taarifa za uchambunzi yakinifu kwa ajili ya kuhuisha mtaala wa watoa huduma ya afya ngazi ya jamii kilichofanyika leo jijini Dodoma Katibu huyo amesemakatika sehemu mbalimbali ikiwemo kijiji cha utulo Wilaya ya Mbalali Mkoani Mbeya mpaka sasa ni miaka mitano hakuna kifo cha mama mjamzito na mtoto wa miaka mitano kutoka akuwa na makomandoo ambao wanaweza kutoa elimu kwa jamii na hivyo kusaidia kuzuia magonjwa yanayosababisha vifo vitokanavyo na uzazi.
Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa vifo vitokanavyo na uzazi kati ya akina mama 100,000 ni vifo 556 na kudai kuwa kama kutakuwepo na huduma ya afya ngazi ya jamii kunaweza kupunguza hali hiyo.
“ Katika kufikia malengo ya Tanzania ya uchumi wa kati na viwanda, wahudumu wa afya ngazi ya jamii wanatakiwa kutumika kuwaibua akina mama ambao hawapeleki watoto wao kupata chanjo, na matumizi sahihi ya matumizi ya vyandarua ili kuepuka ugonjwa wa Malaria na hii imeonekana pia katika nchi za afrika kama Ethiophia,Rwanda na zingine’’, amesema Katibu huyo.
Mbali na hayo Dk Mpoki amesema Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya sekta ya afya yenye lengo la kuboresha huduma za afya na kuimarisha afya za wananchi.
Licha ya hayo amewataka wadau kuunga mkono jitihada hizi za serikali na hivyo kubainisha maeneo ambayo watasaidia.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi wa Mafunzo na Wataalam wa Rasiliamali watu Dk Otilia Gowele amesema kwa sasa wanapitia upya mtaala wa mafunzo kwa hudumu hiyo ili kuendana na hali halisi ya sasa na mahitaji katika sekta ya afya.
Amesema tangu kuanza kutumika kwa mataala wa mafunzo ya watoa huduma hiyo mwaka 2015 na kutumika kwenye vyuo 78 hapa nchini, tayari 9,000 wamehitimu mafunzo hayo.