- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAMA SAMIA AAHIDI KUTATATUA KERO ZA WAFANYAKAZI VIWANDANI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema atamuagiza Waziri wa Kazi kufanya ziara kwenye Viwanda mkoani Pwani kusikiliza kero za wafanyakazi.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia wakazi wa Chalinze kwenye uwanja wa Chalinze Polisi ikiwa siku ya pili ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
“Nimesikia nong’ono kuna tatizo la maslahi ya wafanyakazi wanaofanya kazi viwandani sasa hivi lakini nataka niwaahidi kwamba hili nitakwenda zungumza na Waziri wa Kazi afanye ziara ya kupita viwandani ili asikie malalamiko ya wafanyakazi katika viwanda vile” alisema Makamu wa Rais.
Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alisisitiza ahadi ya kuondoa tatizo la maji kwa wananchi wa Chalinze ipo pale pale kwani Serikali ya awamu ya tano imeweka jitihada kubwa kuhakikisha inaondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi, pia alitoa rai kwa vijana kujifunza ufundi na kuongeza elimu ili wawe na sifa za kuajirika, pia alihimiza wananchi wa Chalinze kujiandikisha kwenye mfuko wa Bima ya Afya.