- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MALARIA YAPUNGUA KUTOKA ASIMIA 18.1 HADI 7.3
Dodoma: Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameliambia Bunge leo Ijumaa Novemba 16, 2018 kwamba Maambukizi ya malaria yamepungua nchini kutoka asilimia 18.1 (2008) hadi kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2017.
Kigwangalla ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye hakuwepo bungeni leo.
Dk Kigwangalla amesema juhudi zinazofanyika katika kudhibiti malaria zimezaa matunda kwa kiwango cha kupungua kwa asilimia 50.
Katika swali la msingi Mbunge wa Kibaha (CCM), Silvestry Koka ametaka kujua Serikali ina mkakati gani kukamilisha azma ya kupunguza malaria nchini.
Akijibu swali hilo, Waziri Kigwangalla amesema Serikali ina dhamira na nia ya kutokomeza magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa malaria.
"Serikali imeendelea kutekeleza mikakati muhimu ya kudhibiti malaria, ambayo imependekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)," amesema Dk Kigwangala
Amesema ili kufikia lengo la kupunguza maambukizi katika jamii na hatimaye kutokomeza malaria nchini, Serikali kwa kushirikiana na wadau inatekeleza afua mbalimbali za kinga na tiba.
Amezitaja afua hizo kuwa ni pamoja na kugawa vyandarua vyenye dawa (LLINs) bila malipo ili kuwakinga watu kuumwa na mbu, kupulizia viuatilifu ukoko ndani ya nyumba na kuangamiza viluwiluwi wa mbu.