- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKONDA AYAROGA MAKONTENA YAKE YASHINDWA KUUZIKANA KWA MARA 4
Dar es Salaam: Mnada unaoendesha harakati ya kuyauza Makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul makonda yenye Samani za ndani umeshinda kuyauza kwa mara ya nne mfululizo makontena hayo.
Akizungumza kwenye mnada huo leo Jumamosi Septemba 15, 2018, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya udalali ya Yono, Scolastica Kevela amesema mnada huo umeendeshwa lakini mnunuzi hajapatikana. Kevela amesema hadi sasa bei zinazofikiwa na wateja hazijafikia malengo waliyowekewa. Soma zaidi. :Mbunge ampongeza Waziri Mpango kwa kumshughulikia Makonda
“Ni kweli wateja wanakuja na bei lakini hazijafikia zile ambazo TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wametuwekea kama kodi yao," amesema. Amesema wao kama madalali wataendelea kufanya utafiti wa kuwapata wateja.
Wateja wachache waliokuwa kwenye mnada huo walionekana kutaja bei lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kufikia kiwango kilichowekwa.