Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 8:41 am

NEWS: MAKONDA AWATAKA VIONGOZI MWENDOKASI KUJIELEZA KUSHINDWA KUTATUA KERO YA USAFIRI HUO

Dar es salaam: Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekiri kutofurahishwa na Mfumo wa Uendeshaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka maarufu kama mwendokasi kwasababu ya kushindwa kutatua Kero za Abiria katika mradi huo.

" Sifurahishwi na namna mradi wa mwendokasi unavyoendeshwa kwani matarajio ya Mh. Rais ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri Kwa wananchi wa jiji la Dar es Salaam ikigeuzwa historia kupitia mradi huu."

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo leo Octoba 10 kutokana na kugubikwa kwa kero katika mradi huo.

Makonda ameagiza watendaji wote wanaosimamia mwendokasi awakute stand ya mwendokasi kimara kesho Saa 12:30 asubuhi ili wamueleze ni kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukua huku wakishuhudia kero wanazopitia wananchi.

"Nitumie pia fursa hii kuwaomba radhi wananchi Kwa kero hii na niwaahidi kuwa jambo hili litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni. Tukutane mapema asubuhi mwendokasi kimara" aliongea RC Makonda

Kero hiyo ya MwendoKasi imeanza Juzi baada ya Mradi huo kuanza zoezi la Kuyapima uzito Magari ya Mradi huo, ambapo imesababisha watu kusimama kwenye mzani kwa wastani wa dakika 3 mpaka 5.

Kwaihyo baada ya zoezi hilo la upimaji uzito madereva wemkuwa wanalazimika kutaka kuchukua abiria wachache ili kwenda na Utaratibu waliopangiwa.