- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKONDA AWADHIHAKI WAPINZANI ASEMA HAWANA HATA OFISI
Dar es Salaam: Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewashangaa wabunge wa upinzani wanaokosoa jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli kwa kupinga kila juhudi za maendeleo nchini ilihali wao hata ofisi yao wameshindwa kujenga.
”Niwatake hawa ndugu zetu waache kupinga kila kitu, kwa maana wao wamekuwa wakipinga shughuli zote za maendeleo, kwanza wao mpaka sasa wameshindwa kujenga hata makao makuu yao miaka nenda rudi, wamepanga mpaka leo, lakini wanapinga tu kila kitu,”amesema Makonda
Makonda ameyaeleza hayo leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika hafla hiyo baada ya Mnyika aliyepewa nafasi ya kusalimu wananchi na kugusia suala la demokrasia, kutaka waliobomolewa nyumba kupisha upanuzi huo kulipwa fidia na kudai kuwa wananchi mtaani vyuma vimekaza.
Baada ya Mnyika kumaliza kuzungumza, Makonda amesema anashangazwa na mbunge huyo kutaka wananchi walipwe fidia badala ya kusifia mradi huo.
Amesema licha ya jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli bado kuna watu wanampinga, huku akitolea mfano elimu bila malipo na ununuzi wa ndege.
“Mnamhukumu kuwapatia fedha, mnamhukumu kwa kupanua barabara nane ili msipate tabu ya usafiri. Hivi mnapokaa nyie na akili zenu mnawaza nini, na mbaya zaidi hata ofisi zao pale makao makuu wameshindwa kuzitengeneza,” amesema Makonda.