Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 10:43 am

NEWS: MAKANG'WA KUPATA MAJI.

DOM: Serikali imeahidi kuanza ujenzi wa visima viwili vya maji katika kijiji cha Makang’wa kilichopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma vitakavyogharimu shilingi milioni 165.7 ili kuondoa adha ya maji wanayoipata wananchi kwa muda mrefu.

Ahadi hiyo imefuatia ombi la mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde alilolitoa kwa serikali.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kukagua mahali patakapo chimbwa visima hivyo katibu mkuu wizara ya maji na umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amesema ujenzi huo utaanza wiki ijayo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Lusinde amewashukuru wananchi kwa uvumilivu wao na kusema visima hivyo viwili vikikamilika vitakuwa jibu la uvumilivu waliouonyesha.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Kituo hiki wameishukuru serikali kwa ahadi hiyo na kueleza namna hali ya upatikanaji wa maji ilivyokuwa.

Kwa mujibu wa mhandisi wa maji kutoka mamlaka ya maji saf na usafi wa mazingira(DUWASA)Kashilimu Mayunga amesema mahitaji ya maji kijijini hapo ni lita za ujazo laki 4 kwa siku hivyo endapo kisima kitaweza kuwa na uwezo wa kutoa angalau lita elfu 8500 kwa siku kitatosheleza mahitaji.