- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKAMU WA RAIS ASIMULIA VIONGOZI WA MKOA WA SONGWE WALIVYOMDANGANYA.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesimulia namna viongozi wa Mkoa wa Songwe walivyomdanganya na kufanya ujanja ili asitembelee Wilaya ya Songwe kwa kisingizio cha ubovu wa barabara.
Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara yake ya siku tano, Makamu wa Rais alisema viongozi hao walimdanganya kuwa wilaya hiyo iko mbali na barabara na haipitiki kirahisi.
Alisema viongozi hao akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, walimzuia kutembelea wilaya hiyo kwa kuwa walikuwa wakijua hakuna mradi wa kuzindua, lakini wakasingizia ubovu wa barabara.
Alisema, aliambiwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuwa wilaya hiyo ina barabara mbovu na ni mbali, lakini baada ya uchunguzi alioufanya kupitia vyombo vyake, aligundua sababu ya kutopelekwa huko ni kukosekana kwa mradi wa kuzindua.
Aliongeza kuwa wilaya hiyo ni tajiri ina fursa za uchimbaji wa madini ya dhahabu hivyo kutokuwa na mradi ni udhaifu wa viongozi wa halmashauri na kuwataka wajitathmini kwa kuwa wanaonekana hawajui wajibu wao.
''Aliniambia Mkuu wa Mkoa kuwa Songwe ni mbali na barabara ni mbovu…ni sawa, lakini vyombo vyangu vimebaini kuwa sababu kubwa ni kwamba hakuna mradi wa kuuzindua viongozi mjitathmini,'' alisema Samia.
Katika hatua nyingine, Samia aliwasihi wananchi wa Songwe hasa Halmashauri ya Tunduma kuzaa kwa mpango ili waweze kumudu gharama za masomo.
Samia alimaliza jana ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Songwe kwa kutembelea vituo vya afya, mradi wa maji, shamba la miti pamoja na kuzungumza na watumishi kupitia vikao na wananchi kupitia mikutano.