Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:44 am

NEWS: MAKAMU WA RAIS AGOMA KUZINDUA STENDI KIBAHA

Kibaha: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amegoma kufanya uzinduzi wa Stendi mpya ya mailimoja kibaha iliyopo Wilayani Kibaha mkoa wa Pwani kwa madai ya kuwepo kwa mapungufu kadhaa katika ujenzi wa stendi hiyo.

Kigugumizi hicho kimetokana na kupata wasiwasi wa utekelezaji wa mradi kuwa na baadhi ya mapungufu ambapo amedai baada ya kufanya uchunguzi wiki mbili ama tatu zijazo atakwenda kuuzindua. Akizungumza katika stand hiyo, Samia jana ockoba 28 alieleza, kuna minong’ono wameisikia kuhusu mradi huo hivyo ni jukumu lake kuibeba na atakapo jiridhisha atarudi kwa mara nyingine .

Pia Samia alisema atakutana na mkuu wa wilaya, mkurugenzi na mkuu wa mkoa kuzungumzia suala hilo. “Msishtuke kwa hili ni kawaida kwa kuchukua hatua za aina hii ili kujiridhisha kwa maslahi ya halmashauri, mkoa na watumiaji kijumla “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sikivu na kusikia malalamiko ya wananchi, tumepata malalamiko kidogo kuhusu stand hii, serikali ni ya uwazi na ukweli hivyo sitofungua stendi “alisisitiza Samia.

Samia alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Jennifer Omolo na mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama na wahusika waliohusika kufanikisha mradi huo. Nae waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI ,Selemani Jafo alisema yeye kama waziri wapo wataalamu wanaohakiki lakini ameridhishwa na kazi hiyo .

“Kwani kila kazi ina changamoto za kibinadamu, hasi na chanya, lakini wamejitahidi “alisema Jafo. Jafo alieleza, mradi huo umepata msaada wa mkopo nafuu kutoka bank ya Dunia ambao wamepata fedha za kimarekani dollar milioni 255 .# Alielezea , wanagusa miji 18 na wanachokifanya wanagusa stendi tisa, barabara za miji kwa kiwango cha lami na madaraja makubwa ya kisasa.