- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAKAMU RAIS WA MAREKANI AMUONYA KIM ASIJE KULETA JANJA JANJA
Washington: Marekani bado inamashaka ikiwa mkutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Koera Kaskazi Kim Jong -un utafanyiaka na kuleta muafaka kati yao kama wanavyo kusudia.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence amemuonya Kim kuwa asimchezee Rais Donald Trump ikiwa watakutana mwezi ujao.
"Yatakuwa ni makosa makubwa kwa Kim Jong-un kufikiri kuwa atamchezea Donald trump," Bw Pence alisema wakati akihojiwa na kituo cha Fox News.
Bw Pence pia alisema kuwa Bw Trump anaweza kuondoka kwenye mkutano huo wa Juni 12.
Kauli ya Pence inaonesha kuwa ni dhahiri Marekani bado inawasiwasi juu ya kitakachofanyika baina ya mataifa hayo mawili katika mkutano huo ujao.
Korea Kaskazini imetisha kujitoa katika mkutano huo baada ya matamshi ya mshauri wa masuala ya ya ulinzi nchini Marekani John Bolton.
Korea Kaskazini ilijibu vikali walati Bolton alisema kuwa itafuata mfumo wa Libya katika kuondoa zana za nyuklia.
Kingozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi alikubaliana na mataifa ya Magharibi mwaka 2003 kuharibu mpango wake ili apate kuondolewa vikwazo. Miaka minane baadaye aliuawa na waasi walioungwa mkono na nchi za Magharibi.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ana mpango wa kukutana na Bw Trump mjini Washingiton leo Jumanne kuzungumzia mipango ya mkutano huo.
Bw Pence alisema hakuna shaka kuwa Bw Trump ana nia ya kuondoka kwenye mkutano huo ambao unapangwa kufanyiwa nchini Singapore
"Sifikiri kuwa Rais Trump anafikiri kuhusu sifa, anachofikiri ni kuhusu amani," Pence alisema.
Gazeti la New York Times liliripoti Jumapili kuwa Trump alikuwa ameulizwa na wasaidizi na washauri wake ikiwa anaweza kuendelea na mkutano huo.