- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAJIBU YA ALIKIBA BAADA YA KUALIKWA NA DIAMOND KWENYE TAMASHA LA WASAFI
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania ALI SALEH KIBA maarufu kama Alikiba ameshukuru kwa mualiko aliopewa na Mwanamuziki mwezake Mkurugezi wa kampuni ya Wasafi Naseeb Abdul maarufu kama DiamondPlatnumz ila amesikitika kwa kutoshiriki katika tamasha hilo la Wasafi festival 2018 linalopangwa kutimua vumbi tarehe 24 mwezi huu kutokana na kutingwa na majukumu ya kikazi.
"ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine." Amesema Alikiba
Lakini Alikiba ametoa ofa ya kudhamini katika kuweka tangazo lake la bidhaa ya Mofaya katika tamasha la Wasafi kama njia ya kushiri katika tamasha hilo.
"Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa"
"Management RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa"
Mwishoni mwa wiki iliyopita November 5, 2018 Diamond kupitia mkutato wake na waandishi wa Habari alimuomba msanii mwezake Alikiba kushiriki katika tamasha la Wasafi Festival 2018
"Natamani kaka yangu Ali Kiba naye awepo na ninaamini uongozi wangu utaanza mazungumzo naye na huko alipo kama anafuatilia wasafi ajue tungehitaji uwepo wake, kwani inabidi tutoke kwenye muziki wa mabifu na tuingie katika kutengeneza hela na kuisaidia jamii inayotuzunguka," alisema Diamond.
Diamond alisema kwa kuanzia tamasha hilo lenye kauli mbiu ya 'Mchezo usiuchezee wewe Kabisa' litafanyika mkoani Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona.