Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:49 pm

NEWS: MAJAJI WASUSIA KESI YA KUHAIRISWA KWA UCHAGUZI KENYA

Nairobi: Majaiji wa mahakama ya Juu nchini kenya (Supreme court ) leo wameshindwa kutokea kusikiliza kesi iliyofunguliwa na wapiga kura watatu waliotaka kuahishwa kwa uchaguzi wa marudio utakao fanyika 26 .10.2017, kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo juma tano 24.10.2017 na Jaji mkuu Davidi Maraga ikiwa yamesalia masaa machache kuingia kwenye uchaguzi wa marudio baada ya mahakama hiyo kufuta matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8. mwaka huu.

Mahakama imeshindwa kusikiliza kesi hiyo kutokana na kuwepo na majaji 2 kati ya majaji 7 hivyo kushindwa kusikiliza kesi hiyo


Jaji mkuu nchini kenya David Maraga siku ya jumanne alisema atasikiliza kesi iliyofunguliwa na raia watatu ambao ni Khelef Khalifa, Samuel Mohochi na Gacheke Gachihi ambao walitaka kuahirishwa kwa uchaguzi huo kulingana na mazingira ya sasa nchini kenya hayaruhusu kufanyika kwa uchaguzi

Kenya inatarajia kuingia kwenye uchaguzi wa marudio kesho alhamisi (26.10.2017) huku upanda wa muungano wa upinzani nchini humo NASA wakipinga kufanyika kwa uchaguzi huo kwa madai ya tume ya uchaguzi nchini kenya IEBC kutofata matakwa yao, yakutaka kuundwa upya kwa taasisi hiyo.