Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:36 pm

NEWS: MAHAKAMA YAWAFUTIA DHAMANA FREEMAN MBOWE NA ESTER MATIKO

Dar es salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia dhamana Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko kwamaana hiyo kuanzia sasa watarudishwa Rumande mpaka pale kesi itakapoisha.

Uamuzi huo unatokana na maombi yaliyotolewa na upande wa mashtaka Novemba 12, uliodai washtakiwa hao wamekiuka masharti ya dhamana kwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama na kushindwa kuripoti katika kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala.

Upande wa mashtaka ulifikia hatua hiyo baada ya Mbowe kushindwa kufika mahakamani, Novemba Mosi na 8 na Matiko kushindwa kufika Novemba 8, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali wa kesi inayowakabili.

Ni Kesi Na. 112/2018 inayowakabili baadhi ya Viongozi Wakuu wa Chama na Wabunge 7 wa Chama Mahakama Kisutu, ambapo washtakiwa watasomewa maelezo ya awali na Hakimu kutoa maamuzi ya dhamana ya mshtakiwa na. 1 na 5.

Mbowe, Matiko na wenzao saba wanakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani hapo yenye jumla ya mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi na uchochezi wa uasi.