- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YATUPIA MBALI PINGAMIZI LA SEREKALI KESI YA MBOWE
Dar ea salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matico wamefanikiwa kupata ahuweni ya rufaa ya dhamana yao baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kukubali kusikiliza rufaa hiyo na kutupilia mbali pingamizi lilowekwa na Jamhuri toka jana.
Wamevuka kihunzi cha pingamizi la Serikali baada ya Mahakama kutupilia mbali hoja za pingamizi hilo.
Katika uamuzi wake leo Ijumaa Novemba 30, 2018 Jaji Sam Rumanyika amekataa sababu ya pingamizi la Serikali kuwa liko mahakamani isivyo halali.
Jaji Rumanyika amesema rufaa hiyo iko mahakamani kihalali kwani si lazima kutaja kifungu cha kisheria kinachochapishwa ambao inasomeka vizuri.
Pia Jaji Rumanyika amekubaliana na hoja ya pingamizi la Serikali sababu mbili za rufaa za kupinga masharti ya dhamana zinakiuka matakwa ya sheria kwa kuwa zimekatiwa rufaa bila kutoa kwanza taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga masharti hayo ya dhamana yaliyotolewa kati ya Machi na April.
Hivyo Jaji Rumanyika amepanga kusikiliza rufaa hiyo saa nane mchana huu.
Mbowe na Matiko ambaye ni mbunge wa Tarime mjini, wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili lakini Serikali iliwasilisha pingamizi la awali ikitoa sababu tatu za kutaka rufaa hiyo itupwe pamoja na mambo mengine ikidai rufaa hiyo iko mahakamani isivyo halali kwani inakiuka vifungu vya sheria.