- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YAMUACHILIA HURU MBUNGE ZITTO KABWE
Dar es Salaam: Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe Leo Novemba 2, 2018 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.
Akizungumza mahakamani hapo wakili wa Serikali, Tumaini Kweka amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi kuwa mshtakiwa hiyo ametenda makosa hayo Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari. Zitto alikamatwa na polisi juzi Oktoba 31, 2018 akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam na kwa nyakati tofauti kuhojiwa katika kituo cha Polisi Oysterbay, Mburahati na baadaye Kituo Kikuu cha Polisi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Zitto aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja atakaesaini bondi ya Sh10 milioni.
Akizungumza mara baada ya kupatiwa dhamana, Zitto Kabwe amesema βkesi za namna hii wamefungwa wakina mandela, na mwalimu kwa hiyo sio jambo linapaswa kuwatisha watu. Ila nasikitika sana jana sikushiriki kongamano la chuo kikuu cha Dar es salaam.β
Aidha amesema βNaamini lazima tuweze kutoa tafsiri mbadala juu ya kile kilichotokea jana, pia niwatake watanzania tuwe na mshikamano ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa imara.β
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12, 2018.
Zitto alikamatwa na polisi jijini Dar es Salaam, siku moja baada ya Polisi mkoani Kigoma kumtaka awasilishe vielelezo juu ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari Jumapili iliyopita Oktoba 28, 2018 kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100 kuuawa katika tukio la mapigano ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi wilaya ya Uvinza mkoani humo. Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amesema tuhuma za mbunge huyo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasi