- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAHAKAMA YA KENYA YAMPA USHINDI UHURU KENYATTA
Nairobi: Mahakama ya Juu(Supreme court ) nchini Kenya imetupilia mbali kesi mbili zilizokuwa zimefunguliwa kupinga uchaguzi wa marudio uluimpa ushindi wa mara ya pili Rais Uhuru Kenyatta.
kwa uwamuzi huo sasa Rais Kenyatta anatarajiwa kuapishwa Jumanne ya wiki ijayo.
Jaji Mkuu David Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.
Kesi ya zilifunguliwa na wananchi wawili ambao ni mbunge wa zamani Bw Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif zimetupiliwa mbali.
"Uchaguzi wa 26 Oktoba umedumishwa, sawa na ushindi wa Bw Kenyatta. Kila upande utasimamia gharama yake," amesema.
Uamuzi wa kina utatolewa katika kipindi cha siku 21.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais wa marudio akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Kiongozi wa upinzani Raila odinga aliyesusia uchaguzi huo alipata kura 73,228 sawa na asilimia 0.96.