Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 10:39 pm

NEWS MAHAKAMA YA JUU LIBERIA YAKWAMISHA UCHAGUZI WAURAIS

Mahakama ya juu nchini Liberia imesitisha maandalizi ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kufuatia madai ya udanganyifu kutoka kwa mgombea aliyeondolewa kutoka kwenye uchaguzi huo.

Mcheza soko Bora Duniani George Weah na makamu wa Rais Joseph Boakai wanatarajiwa kukutana katika duru hiyo ya pili ya uchaguzi tarehe 7 Novemba.

Lakini mgombea wa chama cha Liberty Charles Brumskine, ambaye alichukua nafasi ya tatu amepinga matokeo hayo.

Uchaguzi wa mwezi uliopita ndio wa kwanza huru kufanyika tangu kukamilika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003.

Mahakama imeamrisha chama cha Liberty na tume ya uchaguzi nchini humo kupeleka kesi zao ifikapo Alhamisi.

Lakini msemaji wa tume ya uchaguzi Henry Flomo aliambia BBC kuwa hajajulishwa rasmi kuhusu amri hiyo ya mahakama.

Waangalizi wa kimataifa wakiwemo wale kutoka muungano wa Ulaya hahawajaelezea hitilafu yoyote wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi.