Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 3:35 pm

NEWS: MAHAKAMA KUU YA MAREKANI YAPITISHA MARUFUKU YA TRUMP JUU NCHI 8 ZA KIISLAM

Washington: Mahakama Kuu ya Marekani hatimaye imeidhinisha agizo la lilotolewa na Rais wa marekani Bw. Donald Trump kuhusu marufuku usafiri kwa raia kutoka nchi zenye Waislamu wengi. Katika uamuzi wa siku ya Jumatatu, Desemba 4, Mahakama ya Juu nchini Marekani iliruhusu kutekelezwa kwa agizo la rais Trump, licha ya kuwepo kwa rufaa zingine katika mahakama za chini.

Rais Trump alirekebisha agizo lake mara tatu na kila wakati jaji aliingilia kati kuzuia utekelezaji wake. Lakini siku ya Jumatatu, Mahakama Kuu nchini Marekani ilithibitisha kuwa agizo hilo liko sahihi: Mahakama Kuu iliruhusu utekelezaji kamili wa toleo la hivi karibuni la agizo hilo.

Ni marufuku kwa raia wa nchi nane kusafiri kwenda Marekani. Mwezi Oktoba, majaji wawili wa Marekani waligundua kwamba agizo hilo lina kasoro na ubaguzi wenye misingi ya utaifa. Majaji saba wa Mahakama Kuu kati ya tisa wameamua agizo hilo lianze kutekelezwa , lakini hawakuelezea uamuzi wao.

Hata hivyo, Waislamu, kutoka Libya, Somalia, Chad, Yemen, Syria, na Iran hawataweza kupata visa kwenda Marekani, hata kama wana uhusiano wa familia na watu waishio kisheria nchini Marekani. Korea Kaskazini na Venezuela pia zinahusika, lakini marufuku dhidi ya raia kutoka nchi hizi mbili tayari ilipitishwa na majaji hivi karibuni.

Majadiliano Zaidi yatendelea kusikilizwa wiki hii katika mahakama huko San Francisco, California, na Richmond, Virginia.