Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:50 pm

NEWS: MAGUFULI ATOA SABABU YA KUTO TENGENEZWA MBADALA YA MV BUKOBA

Mwanza. Rais John Magufuli amesema kuwa alipofikiria na kutangaza uamuzi wa kujenga meli mpya ambayo ni mbadala wa meli kubwa ya MV Bukoba itakayosafirisha abiria na mizigo baina ya Mwanza na Bukoba aliingiwa na hofu ya kutofanikisha lengo hilo.

Ameongea kauli hiyo leo Sept 3, 2018 wakati akihutubia muda mfupi baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli nyingine mbili,

Kwanini aliingiwa hofu

Rais Magufuli amesema kilichomtia hofu ni swali la kwanini marais waliomtangulia kama Rais Mkapa, Kikwete walishindwa kujenga meli mpya miaka 22 tangu meli ya Mv Bukoba ilipozama mwaka 1996.

"Lakini leo hii nafarijika kushuhudia utiaji saini wa ujenzi wa meli mpya kwa fedha za kodi ya Watanzania," amesema Rais Magufuli. Amesema ujenzi wa meli mpya si tu utarahisisha usafiri na usafirishaji kati ya mikoa ya Mwanza na Kagera, pia utapunguza gharama za kusafirisha mizigo. Ametoa mfano wa gharama ya kusafirisha tani moja ya mizigo itakavyoshuka kutoka Sh60,000 hadi Sh